KONDOO ALIYEPATIKANA

Na Brian Nzomo

Nilipofika, nyimbo za kumwabudu mungu zilisheheni hisia za waumini. Niliketi nyuma. Sikujihusisha na shughuli hizo za kunyenyekea kwani zilinikalia kama matendo butu. Kando yangu, mzee mmoja aliboboja maneno shaghalabaghala. Hii ndio lugha iliyotajwa kuwa ya kiroho na haikueleweka na masikio ya binadamu kwa hali ya kawaida. | Bright News



Sikujua ni jambo lipi lililonipeleka kanisani Jumapili hiyo, wala sikuelewa ari hiyo ilinigubuka vipi. Miaka kumi sikupata kutia miguu yangu katika maabadi yoyote. Shughuli mzo, safari za hapa na pale na anasa za dunia zilinimeza zote nikasahau kuitenga angalau siku moja kumshukuru mungu kwa “neema zake”.

Hapo mwanzoni kabla ya kupotoka kwangu, nilikuwa mja msalihina na kijulanga aliyemcha mungu si kidogo. Nilizifuata amri zake kama mkomunisti mtiifu wa Uchina. Niliwahusudu sana watumishi wa mungu. Waliozungumza kwa ukweli na roho. Waliolipua maombi mazito, mafundisho yaliyonigusa roho kwa kiasi cha kupukutikwa machozi. Siku zile, nilikongamana na Wakristo wenzangu vijana wa hlrimu yangu katika mijadala ya kiroho. Chini ya maembe ule uliokuwa nyuma ya jengo la kanisa, tulijadili kwa muda mrefu kuhusu maudhui ya kindani ya neno la mungu. Kila mmoja wetu amevalia kinadhifu. Binti waliokuwepo walivalia marinda marefu na vibwebwe vichwani. Nyuso zao ziling’aa kwa mafuta ya kawaida. Hamna vipodozi vingine vilivyotajwa kuwa vya kishetani.

Wakati huo, nembo iliyoitawala maisha yangu ilikuwa moja tu. “Chochote kisichompendeza mungu, hakistahili kutiwa mawazoni “. Nilijaribu kwa udi na uvumba kufuata njia za uadilifu na kumweka shetani pembeni asije akauharibu uhusiano wangu na Yesu. Lakini ujana hauchechei kwa ushawishi. Niligundua kuwa nilimpenda binti mmoja pale kanisani. Tatizo ni kuwa alikuwa ashaolewa na mwenyekiti wa miradi kanisani. Niliomba na kusali kwa siku tatu mfululizo ili kuondoa mawazo machafu yaliyoanza kuivamia akili yangu.

“Rudi nyuma yangu eeh Ibilisi,” niliomba. Lakini wapi! Kila nilipomwona na kuzama katika lindi la tabasamu yake changamfu, ashiki za mapenzi zilinimiliki. Si mara moja au mbili niliota nikishiriki naye kimapenzi. Si kitandani, si kichakani, hadi mawinguni. Nilihisi kuemewa na hisia kinzani zilizonipapa siku baada ya siku. Hisia ya uchu wa mapenzi na hisia ya shutuma dhidhi ya uovu ulionibanza.

Nilimweleza pasta shida niliyokuwa nayo. Hakusema mengi. Alisema kwa ufupi,
“Usimpe shetani funguo za maisha yako. Wiki ya ngapi hii umekosa vikao vya kuchambua bibilia kwa masingizio ya kazi? “

“Tatu,” nilisema kwa soni. “Haya basi! Waona? Hapo ndipo Ibilisi alianza kukutawala na fikra za kipumbavu….”

Nilidhamiria kumwepuka Zara Mkocho ila haikuwa rahisi. Kila nilipokusudia kumwondoa mawazoni, ndivyo nilivyojiponza. Moyo ukapata maumivu zaidi. Zara mke wa watu akawa amening’ata kwa sirihi zake.

Jioni moja nilikuwa kanisani nikitayarisha mafunzo ya siku itakayofuata. Nilikuwa nimechoka tiki! na mara kwa mara nilihisi kusinzia. Niligutuka pindi mkono laini ulinigusa shingoni. Nilipomtazama aliyenigusa, nilipapwa na moyo. Zara Mkocho alinitazama huku akitabasamu. Kisha akaniambia,

“Naona una kazi nyingi Leo, ungependa nikusaidie…” Niliemewa kwa mughma nikashindwa kuongea . Hakusema lingine lolote bali akileta kando yangu na kudadisi karatasi nilizokuwa nikiandika. Joto uliozizima kwa kiungo chake, manukato yaliyohanikiza chumba kizima na urembo wa nguva; vyote viliniweka katika hali isiyo ya kawaida. Ilionekana kuwa aligundua kutotulia kwangu.

“Kwani waniogopa?” Aliuliza huku akinigusa mkono. Mama yangu! Nikawa kama mgonjwa wa kifafa na pumu. Nilizizimwa si kidogo. Joto ikanipanda kwa hasira. Nilitamani mlango ungekuwa wazi nipate upenyu wa kutorokea . Lakini wapi! Niliketi tuli huku maungo yangu yamegoma kazi. “Tulia mwana! Usiniogope miye. Miye ni mwanamke tu. Kiumbe mwenzako. Mwenye damu na hisia sawia na zako…” Alisema huku akinipapasa pajani. Yule bwana mwingine kule chini akaanza kupata ufahamu. Amehisi kuwa kitoweo ki karibu.

Zara alisimama na kuelekea mlangoni. Alitazama nje na kwa kweli giza ilikuwa imeanza kuingia. Akaufunga mlango kwa komeo na mara moja, akaudondosha rinda lake la kitenge. Nikaachama. Ebo! Binti kaumbwa kaumbika. Akanikaribia nilikokaa. Akanikalia mapajani na kutumia mikono yangu, akaifungua sidiria yake na kuibwaga sakafuni. Madodo yaliyo mbivu yakanitazama yakinisihi niyakande na niyachezee jinsi mtoto achezeavyo pute. Aliivuta uso wangu na kuuzamisha katika kifua chake kwa nguvu. Ulimi wangu nao ukaanza kazi. Akaghuna. Akalia kwa furaha. Nami nikahisi nimetekwa kabisa siwezi nikarejea nyuma.

Jamani, Yusufu alimwepuka vipi mke wa Potiferi? Nikaomba kimoyomoyo mungu aniepushe na majaribu haya yaliyonisabilia. Lakini nilipomwiingia Zara, nilijua wazi kuwa nimeshindwa vita. Shetani akacheka kwa kejeli akilini. “Lo, amewezwa.” Sikuwa na budi ili kumaliza kazi niliyoianza. Lakini utamu wake Zara…

Nilidhamiria kumwepuka Zara Mkocho ila haikuwa rahisi. Kila nilipokusudia kumwondoa mawazoni, ndivyo nilivyojiponza. Moyo ukapata maumivu zaidi. Zara mke wa watu akawa amening’ata kwa sirihi zake.


**** ***** ****

Nilidhani kuwa kosa nililofanya litasalia katika himaya ya kale isiyokusudiwa kurejelewa. Sitamtamani Zara tena, nilijiambia. Lakini matukio ya jioni ile yalicheza akilini mwangu kama kanda la ngono isiyofutika. Naye Zara hakuchesha kunitafuta kwa kusudio la kunishinikiza kuyatenda tuliyoyatenda. Nikawa kondoo wake. Sikupata nguvu ya kukataa na kulikomeza shinikizo lake. Nilibugiwa mzima mzima na pepo la usherati.

Ningesahau vipi kuwa Zara mwenyewe ndiye alinipeleka kilabuni kwa mara ya kwanza? Kuwa ndiye aliyeninulia kileo kilichoitwa ‘Konyagi’ ? Zara mwenyewe ndiye aliyenikosha akilini kwa mbinu elfu za kushiriki mapenzi? Kwangu, Zara akawa kungwi wa anasa za dunia. Nilishangazwa si kidogo na jinsi alivyokuwa mahiri wa kuficha maisha yake haya kwa kiasi kuwa mumeye na kanisa walimjua kuwa mwanamke mwadilifu asiye na hila wala uchafu. Walimwona malaika. Gizani miye, nilimwona ibilisi mshawishi. Na nilimpenda zaidi hivyo.

Njia ya mdanganyifu ni fupi. Pasta mwenyewe ndiye alitufumania uchi katika maktaba ya kanisa. Nilijawa tahayuri. Lakini Zara hakuonekana kuwa na wahaka licha ya kuwa hilo lingemfisadi jina na kuhatarisha ustawi wa ndoa yake na mumeye. Huenda sikumjua vyema ibilisi huyu. Zara hakuwa na kazi ngumu kumloweza mumewe kwa masikitiko yake ya uongo. Bwana Chamela akajawa huruma. Moyo wake ukatoneshwa kwa maneno ya Zara, akamsamehe na kuahidi kulisahau tukio hilo. Nami nikaagizwa niondoke pale kanisani nisije nikawaharibu binti za watu. Nilitamaushwa mno. Nikaapa kutotia guu langu katika kanisa lolote lile. Anasa na kazi zikawa ibada yangu. Miaka kumi baadaye, umri wangu thelathini. Sina mchumba wala mke. Narejea kanisani. Hamu ya familia imeanza kuniafiki. Nipo katika safari ya kumtafuta mke mkristo aliyetosha. Mtulivu, mwadilifu na asiyechechea kwa taadhima.

***** ****** *****

Kanisani. Nilipofika, nyimbo za kumwabudu mungu zilisheheni hisia za waumini. Niliketi nyuma. Sikujihusisha na shughuli hizo za kunyenyekea kwani zilinikalia kama matendo butu. Kando yangu, mzee mmoja aliboboja maneno shaghalabaghala. Hii ndio lugha iliyotajwa kuwa ya kiroho na haikueleweka na masikio ya binadamu kwa hali ya kawaida.

Msichana aliyekuwa kando yangu upande wa kushoto alikuwa na wajihi wa mvuto. Alipukutikwa machozi, vile vile aliboboja kwa maombi mazito ya kiroho. Nilikiinamisha kichwa changu ili nisionekane mgeni. Nikahisi kuchoshwa. Sikuelewa ni namna gani nilivyowahi kuipenda ibada ya kanisa. Wala sikutaka kukumbuka kuwa kuna wakati ambao niliwahi kutekwa katika ulimwengu wa kikristo namna hii. Nilicheka moyoni nilipokumbuka kuwa shetani alifaulu kuniondoa katika orodha ya wanakondoo wa Kristo. Nilijitonesha hata hivyo. Iwepo mungu mwenyewe ndiye aliyeniumba na mwili huu usiojua maovu. Mwili wenye uchu wa kukiuka maagizo yake, basi anaye makosa ni nani?

Kanisa la “Jesus loves ministries” lilikuwa kanisa lililopendwa na watu wa tabaka la kati. Kanisa hili lilikuwa na idadi ya waumini mia saba. Mtumishi mkuu Kasisi Desmond Karanji alilianzisha kanisa hili miaka ishirini iliyopita. Wakati huo, kanisa lilikuwa na waumini takriban mia moja na lilikuwa kibanda cha mabati katika eneo duni la Kiberi. Nilimtazama kwa kina. Miaka kumi imepita tangu kumtumbulia machoni. Amekonga na kubugia chumvi na mvi ulimkaa kichwani kama uga wenye theluji. Usoni makunyanzi na vimbimbi vya uzee vimetamalaki. Lakini alionekana kuwa mkwasi zaidi. Alivaa suti ya buluu lenye dhamani. Huenda ilikuwa suti ya lasi. Kiwikoni alikuwa na saa ya sababu. Vidoleni pete za dhahabu vilevile.

Baada ya nyimbo za sifa, ukumbi mzima ulinuka jasho na kusheheni joto jingi. Tuliagizwa tuketi ili kuwasikiliza kwaya. Baada ya hapo, tungetoa sadaka na zaka zetu ili mhubiri atupe neno la Bwana.

Kwaya ilinisinya kweli. Waliimba kwa sauti zilizozingua masikio. Mara kwa mara walikinzana maneno na hawakufuata mahadhi ya ala. Lakini makofi yalikuwa mazito. Msimamizi wa ibada akawapa kongole na kusema kuwa kwaya hiyo iliwapiku wengine katika kughani nyimbo za kumtukuza mungu.

Kikapu cha sadaka kiliponifikia, nilitoa noti ya shilingi Mia moja mfukoni na kuitosa ndani. Waumini waliokuwapo karibu wakanitazama kwa mwao. Mja yupi huyu aletaye shilingi Mia moja katika kanisa lenye nafasi kama hili? Mle ndani kikapuni, noti za hudhurungi (elfu moja) ziliendelea kuwa mzo .

“Bwana Yesu asifiwe!” Mkewe pasta alisimama na kusema kwa wingi wa nishati.

“Asifiwe tena na tena!” Umati ulisema kwa nguvu. “Haya basi wateule wa mungu. Hii leo tuna bahati kumkaribisha tena kondoo wetu aliyepotea hapa karibu mwongo mmoja uliopita. Bwana Anselm Okata…” Nikashangaa. Walijua vipi nimerejea. Aaah!Sharti waliniona kwenye maegesho nilipigwa Prado yangu. “Bwana Anselm. Hebu njoo mbele uisalimie kanisa na utupe ushuhuda wako. Umekuwa wapi, na una lipi la kutueleza kuhusu jinsi Yesu alivyokuonekania wakati wote huo …” Nilisimama na kuelekea mbele ya kanisa. Nikatazamana na macho Mia saba. Waume kwa wanawake. Wazee kwa vijana. Wakuu kwa watoto. Wote wanasubiri niwape uongo.

Nilijikohoza kidogo na kuanza, “Bwana Yesu asifiwe… Jina langu ni Anselm Okata. Nilikuwa mshiriki wa kanisa hili miaka yapata kumi iliyopita. Mimi ni mfanyibiashara mashuhuri . Nina kampuni ya mawasiliano na kiwanda cha vileo…”

Nikaeleza kwa kina kuhusu azma yangu ya kutaka mchumba. Na kuwa nimeona mwanga. Anasa za kilimwengu hazifai . Hakuna raha halisi katika nyuga za kilimwengu. Raha iliyo dumu ipo ndani ya Yesu. Na kuwa nilihitaji mwenza na familia halisi katika safari ya uaminifu.

Ukemi wa furaha ukapigwa. Kondoo amerejea. Amerejea kwake mchungaji mkuu Yesu Kristo. Ambapo mna raha tele. Hamna kilio wala taabu. Kasisi Karanji akasema kuwa kumiliki kiwanda cha Pombe hakukunitenga na Yesu. Na kuwa ilikuwa kazi tu. Hata Mathayo alikuwa mtoza ushuru. Alikuwa mfisadi vile vile kama Zakayo mbilikimo. Na kuwa iwepo nitakuwa muumini mwema asiyesita kumtolea mungu zaka, hayo yote yangefutwa.

Baada ya ibada hiyo iliyolenga sana ustawi wa kifedha, kasisi Karanji aliniita chemba na kunidokezea kuwa nisiwe na wasiwasi . Mke nitampata bila tatizo. Mumo kanisani mlikuwa na vidosho waadilifu wa kutosha. Aliahidi kunifanyia mipango kamili ya kumpata mmoja. Sikusema neno.

Nilizokuwa nikiondoka ofisini mwake, nilipishana naye Zara. Alikuwa amenenepa zaidi na urembo wake wa awali ulikuwa umefifia . Hata hivyo alionekana kuvutia na mwenye bashasha kama hapo mwanzoni.

Aliniamkua kwa furaha. Nami nikamwaamkua pia. Nikazungumza naye kwa kusudio la kumvuta katika mahusiano yetu wa jadi . Akasema kwa kweli ameokoka na kuwa hangependa kurejea hulka zake za hapo mbeleni. Alikwisha pewa talaka na mume wake. Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano na alikuwa na watoto wawili. Hakutaka mchezo. Alitaka mume wa kikweli . Mcha mungu na asiyechelea majukumu. Nilitikisa kichwa tu. Machoni pake hata hivyo niliona ishara ya fundo chungu moyoni mwake. Nikaamua kumwaga.

“Na si unipe namba zako za simu,” alisema nilipoanza kuenda. Nikasubiri kidogo. “Namba zangu ufanyie nini?” Nilitaka kuuliza. Hata hivyo nilikata ushauri nikampa. “Ningependa sana tukutane tuzungumze…” aliniambia. Sikusema neno. Niliondoka pale. Akilini hata hivyo mlikuwa na maswali chungumzima. Alitaka nini Zara? Na je, matukio ya kale yangejirudia tena? Hapana! Nilijisemea. Haiwezekani. Zara alitaka mume. Huenda alitaka nimwoe? Kuna uwezekano.

Sikumbuki nilisimamishwa njiani na watu wangapi waliotaka kuniamkua. Wengi wao walikuwa mabinti. Walitaka tubadilishane anwani. Wengine wakanirai nijiunge nao katika mazoezi ya kwaya au majadiliano ya bibilia. Kila mmoja nikawaahidi wakati wangu. Nikaondoka mle kanisani nimeghafilika mno.

La hasha! Niliapa. Siwezi nikampata mke au lolote la maana kutoka kanisa hilo. Nitarejea kwa ibada niijuayo. Anasa.

Brian Nzomo ni mwandishi na mwanafunzi wa mawasiliano na uanahabari katika Chuo kikuu cha Kenyatta. Wasiliana naye kupitia anwani ya barua pepe: bryonzoms505@gmail.com

Design a site like this with WordPress.com
Get started