Na Brian Nzomo. Machozi yakapukutika bila amri au tamanio langu. Sikutaka kuyafuta. Yatiririke tu! Kuna mengi yamtafishayo binadamu. Huzuni, penzi lililotawanyika, usaliti, ugomvi, uchungu na kutowajibika ipasavyo. Ila, ipo hali imwekayo kabisa katika lindi la taabu kama njaa?Njaa, si ya chochote kingine bali ile ya tumbo ihitajiayo chakula.Nilipokuwa katika mwaka wangu wa pili katika chuoContinue reading “UPWEKE WA TAABU.”
Tag Archives: fasihi
GRESI.
Na Brian Nzomo. Wanafunzi wa darasa la sita walichoshwa na chuki niliyokuwa nayo dhidhi ya Gresi. Gresi alikuwa banati aliyesomea darasani kwetu ila alikuwa amepevuka kiumri kumpiku mwanafunzi yeyote yule. Alikuwa na umri wa miaka kumi na mitano, wengine wetu tulikuwa na umri wa miaka kumi na miwili. Alikuwa msichana mrefu ajabu mwenye umbo laContinue reading “GRESI.”
KONDOO ALIYEPATIKANA
Na Brian Nzomo Sikujua ni jambo lipi lililonipeleka kanisani Jumapili hiyo, wala sikuelewa ari hiyo ilinigubuka vipi. Miaka kumi sikupata kutia miguu yangu katika maabadi yoyote. Shughuli mzo, safari za hapa na pale na anasa za dunia zilinimeza zote nikasahau kuitenga angalau siku moja kumshukuru mungu kwa “neema zake”. Hapo mwanzoni kabla ya kupotoka kwangu,Continue reading “KONDOO ALIYEPATIKANA”
HUKU SI KWENU
Na Brian Nzomo. “Situmahi kukuona hapa hivi karibuni. Miaka kumi na mitano ni mingi sana. Hata hivyo kuna tumaini. Tumaini ya kuwa utarekebisha mkondo wa maisha yako na kuwa mwananchi mwema na mwadilifu…” alidokeza yule afisa wa magereza akimkabidhi Simiyu shanta lililosheheni nguo zake. Suruali moja mararumararu na shati la buluu lililochanika. Hizo ndizo maliContinue reading “HUKU SI KWENU”
UTENZI WA MWANA KUPONA NA UCHAMBUZI WAKE.
Na Brian Nzomo. Nagema wangu binti,Mchechefu basanati,Upulike wasiati,Asaa ukazingatiya… Utendi wa Mwana Kupona ni mojawapo ya mashairi yanayojulikana sana katika historia ya Kiswahili. Shari hili lilitungwa na mwanamke aliyejulikana kama Mwana Kupona binti Mshamu Nabhany aliyezaliwa katika mji wa Pate mwaka wa 1810. Historia ya maisha yake Mwana Kupona imefafanuliwa vyema na wasomi A. WernerContinue reading “UTENZI WA MWANA KUPONA NA UCHAMBUZI WAKE.”